Josef Stalin

Joseph Stalin
Joseph Stalin

Joseph Vissarionovich Stalin (Kirusi Иосиф Виссарионович Сталин (Iosif Vissarionovich Stalin), kwa jina la kiraia Джугашвили (Dzhugashvili), Kigeorgia: იოსებ ჯუღაშვილი (Ioseb Jughashvili); (* 18 Desemba (katika Kalenda ya Juliasi: 6 Desemba) 1878 – + 5 Machi 1953) alikuwa mwanasiasa Mrusi kutoka Georgia aliyeshiriki pamoja na Lenin katika Mapinduzi ya Urusi ya 1917 na kuwa kiongozi wa chama cha kikomunisti halafu kiongozi mkuu wa Umoja wa Kisovyeti baada ya kifo cha Lenin.

Alitawala Urusi kama dikteta kwa unyama aliyesababisha vifo vya mamilioni ya watu. Alifaulu kujenga uchumi na jeshi la Umoja wa Kisovyeti na kutetea nchi dhidi ya mashambulio ya Ujerumani wakati wa vita kuu ya pili ya dunia. Alikuwa kati ya washindi wa vita kuu ya pili akapanusha utawala wake juu ya nchi za Ulaya ya Mashariki na ya Kati kama vile Poland, Uceki, Hungaria, Romania, Bulgaria na sehemu ya mashariki ya Ujerumani.

Stalin alikubaliwa kama kiongozi wa nchi zote za kikomunisti pamoja na China, Vietnam na Korea ya Kaskazini hadi kifo chake.

Alifuatwa na Nikita Krushchov kama kiongozi wa chama na Umoja wa Kisovyeti.


Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Josef Stalin" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Josef Stalin kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.




SEO Tools wymiana linkami system wymiany linków SEO Tools tanie kredyty gotówkowe kreatyna Plaza 3 star hotel Los Angeles krynica noclegi Sejm Tyk